Thursday, May 24, 2012

nguvu ya ujasiriamali nchini Tanzania

Nchi ya Tanzania inaaminika sana kuelekeza nguvu zake katika kilimo kwa asilimia 80..wajasiriamali wadogo wadogo ndio wamefanikiwa kwa asilimia kubwa kuifikisha nchi katika hali hii ya maendeleo japo sio makubwa sana lakini tuna kila haja ya kujivunia wajasiriamali tulionao hapa nchini.Mimi nikiwa miongoni mwa wajasiriamali wa hapa nchini nina furaha kubwa kuona tunazidi kusonga mbele badala ya kurudi nyuma..katika mambo ambayo naweza kujivunia ni pale napoona hata vijijini wameanza pata funguka macho na pia serikali inaanza kwa mbali kutambua mchango wetu mkubwa katika jamii nzima kwa ujumla..sasa basi naiomba serikali angalau ikubaliane na wajasiriamali na kuendeleza shughuli za uzalishaji kwani maendeleo sio ya mmoja bali ni kwa taifa zima kwa ujumla!!

1 comment:

TAECO said...

ni nguvu ya ujasiriamali iliyoikomboa marekani na china hadi leo hii ndio nchi zinazoongoza duniani kwa utajiri lakini utajiri wake umetokana na wajasiriamali wanaojituma kwa nguvu zote na wenye mshikamano wa hali ya juu!