Wednesday, June 20, 2012

Viashiria vya Kitamaduni vya Maendeleo ya Binadamu:

Kukuza maendeleo ya binadamu na kuheshimu tofauti za kiutamaduni ni changamoto kubwa kwa
Afrika na kwa dunia nzima. Katika mazingira ya sasa mambo matatu ni muhimu katika
kufanikisha lengo hili.
La kwanza ni kubuni rajua (dira) ya pamoja: Afrika haina budi kubainisha rajua yake yenyewe
kwa ajili ya mustakabali wake. Tafiti za malengo ya muda mrefu zilizofanyika katika ngazi ya
kitaifa na kikanda zinaonyesha kwamba rajua ya namna hiyo itajumuisha nyanja mbalimbali za
kiuchumi, kijamii, kisiasa, kimazingira, kitamaduni na kiteknolojia. Katika kila uwanja, mikakati
sahihi haina budi kubuniwa kwa kuoanishwa na malengo ya muda mrefu ya rajua hiyo. Katika
uwanja wa utamaduni, mkakati unaofaa zaidi ni wa ukuzaji wa umoja katika uanuwai kama
unavyohimizwa na Ripoti ya UNDP1 2004 ya Maendeleo ya Binadamu. Mkakati huu hautilii tu
mkazo katika kuvumiliana, bali pia katika kushirikiana miongoni mwa vikundi vya wenyeji
katika ngazi ya kitaifa na ya kikanda. Aidha unadokeza haja ya kuvumiliana na kushirikiana
katika ngazi ya kimataifa miongoni mwa mataifa.
Mchakato wa uundaji wa rajua hiyo hauna budi kupewa umuhimu sawa na matokeo yake.
Mchakato huo hauna budi kuwa shirikishi na jumuishi kwa kadri iwezekanavyo, kama lengo ni
kuwa na rajua yenye kunufaisha wengi na inayomilikiwa na walio wengi pamoja na jumuia
mbalimbali.
Pili, utendaji ni kipengele muhimu na unapaswa uhusishe masuala ya shughuli za utafiti, hatua za
kisera na shughuli za utekelezaji. Shughuli za utafiti hazina budi kushughulikia masuala ya
viashiria vya kitamaduni vya maendeleo na viashiria vya maendeleo ya kiutamaduni. Masuala ya
kisera yatahusu uundaji na utekelezaji wa viunzi ambavyo vitalazimisha kuwapo kwa tathimini
ya ubora wa shughuli za utamaduni. Shughuli za utekelezaji hazina budi kuelekezwa katika
kuhimiza kuingiza sera za utamaduni katika mikakati, sera na programu za maendeleo za maeneo
na za taifa.
Tatu ni tathmini na ufuatiliaji. Hata kama rajua iliyobuniwa itakuwa inatia hamasa na utekelezaji
wake utafanywa vyema, bado maendeleo haya inabidi yatazamwe kama mchakato wa kujifunza
ambao unapaswa kufanyiwa mapitio, marekebisho, na mageuzi ya mara kwa mara. Na ni
muhimu kuhakikisha kwamba wadau wote wanashirikishwa katika mchakato huu wa tathmini na
ufuatiliaji, na kwamba juhudi za makusudi zinachukuliwa kuhakikisha kwamba wote
wanashirikishwa kikamilifu

No comments: